April 16, 2018

NESCH MINTEC Yatoa Semina kwa wachimbaji wa Dhahabu



Wito umetolewa kwa wachimbaji na wafanya biashara ya madini aina ya dhahabu kujenga tabia ya kutumia maabara za kisasa kupima madini hayo kabla ya kuyauza ili kuepuka upoteaji

Mkurugenzi wa Kampuni ya NESCH MINTEC TANZANIA LIMITED ambao ni wataalam wa madini aina zote katika mkutano wao na wadau wa madini kanda ya Ziwa uliofanyika  jijini Mwanza,akieleza jambo.
Wadau wa madini wakiuliza maswali



Mkurugenzi wa Kampuni ya NESCH MINTEC TANZANIA LIMITED Bwana Happines Nesvinga akitoa maelezo katika Maabara ya Kisasa,iliyopo jijini Mwanza.     


Wito umetolewa kwa wachimbaji na wafanya biashara ya madini aina ya dhahabu kujenga tabia ya kutumia maabara za kisasa kupima madini hayo kabla ya kuyauza ili kuepuka upoteaji 

Wito huo umetolewa na Mkurugenzi wa Kampuni ya NESCH MINTEC TANZANIA LIMITED ambao ni wataalam wa madini aina zote katika mkutano wao na wadau wa madini kanda ya Ziwa uliofanyika  jijini Mwanza
Mkurugenzi wa NESCH MINTEC Bw.Happines Nesvinga amesema kuwa wachimbaji wa madini wamekuwa wakiendesha shughuli zao kienyeji hali inayowakosesha mapato na kupeleka kufanya kazi kwa hasara
Insert:- Bw Happines Nesvinga

Nao baadhi ya wachimbaji walioshiriki katika mkutano huo akiwemo Mzee Cosmas Nkayamba mchimbaji wa dhahabu katika kata ya Nyakahula wilayani Biharamulo ammekiri kuwa uchimbaji wa kienyeji unawapa hasara na kuiomba serikali kuwapatia elimu ili kuboresha shughuli zao.       


www.ngarakwetu.blogspot.com

March 1, 2018

Vladimir Putin asema Urusi ina kombora lisiloweza kuzuiwa

Vladimir Putin asema Urusi ina kombora lisiloweza kuzuiwa

Urusi imeunda kombora jipya ambalo haliwezi kutunguliwa na linaweza kufika pahala popote duniani, kwa mujibu wa Rais Vladimir Putin.

Bw Putin amekuwa akieleza sera zake muhimu za muhula wa nne, taifa hilo linapokaribia kufanya uchaguzi katika siku 17.
Rais huyo anatarajiwa kushinda.
Amesema kombora "halipai juu sana, ni vigumu sana kulitambua likipita, lina uwezo wa kubeba kichwa cha nyuklia na linaweza kufika popote pale. Aidha, njia linayofuata haiwezi kutabirika na adui, linaweza kukwepa vizuizi na kimsingi haliwezi kuzuiwa na mifumo ya sasa ya kinga dhidi ya makombora na hata mifumo inayotarajiwa kuundwa siku zijazo."
Katika nusu ya kwanza ya hotuba hiyo yake kwa taifa, ameahidi kupunguza viwango vya umaskini nchini humo.
Kisha, ameonesha mkusanyiko wa silaha mpya, likiwemo kombora alilosema linaweza "kufika pahala popote duniani".
Hotuba hiyo ya Bw Putin imeendelea kwa saa mbili.
Uchaguzi utafanyika mnamo 18 Machi.
   chanzo:BBCSWAHILI

www.ngarakwetu.blogspot.com

December 28, 2017

Wafuasi wa Weah waanza kusherehekea ushindi Liberia

Wafuasi wa Weah waanza kusherehekea ushindi Liberia

Mwanasoka wa zamani wa kimataifa wa Liberia ameanza kutumiwa ujumbe wa kumpongeza hata kabla matokeo rasmi ya uchaguzi wa rais hayajatolewa. Wafuasi wa Weah wanasema mgombea wao amepata zaidi ya asilimia 60 ya kura.
Maafisa wa tume ya uchaguzi hawakuthibitisha taarifa hizo kutoka timu yake ya kampeni, na mpinzani wa Weah, makamu wa rais Joseph Boakai, amelimbia shirika la habari la Reuters kuwa hajaona hesabu zozote za kura na kwa hivyo bado ana matumaini ya ushindi.
Matokeo yasiyo rasmi yaliyotolewa na vyombo vya habari vya ndani yameendelea kumuonyesha Weah, mchezaji wa zamani wa klabu za AC Milani na Paris Saint-Germain, akiwa mbele katika kura hiyo ya duru ya pili, ambayo inanuia kuleta mabadiliko ya kwanza ya kidemokrasia tangu mwaka 1944.
Tume ya uchaguzi ya Liberia ilisema ingetangaza matokeo ya kwanza jioni ya Alhamisi, ingawa mchakato huo umekumbwa na ucheleweshaji. Kituo cha Carter cha nchini Marekani kimesema kumekuwepo na maboresho kadhaa katika usimamizi wa kura ya Jumanne kutoka ile ya mwanzo iliyofanyika mwezi Oktoba, kikirejea tathmini chanya iliyotolewa na waangalizi wengine wa kimataifa.
 Liberia Wahlen Joseph Nyuma Boakai (Reuters/T. Gouegnon) Mpinzani wa Weah, makamu wa rais wa sasa Joseph Boakai anasema bado ana matumaini ya ushindi.
Katibu Mkuu wa chama cha Weah, Janga Kowo, amesema wanatumai kupokea simu ya pongezi kutoka kwa Boakai ingawa hawajasikia chochote kutoka kwake mpaka sasa. Kowo amesema takwimu za timu yake zimekokotolewa kutoka asilimia 60 ya kura zilizopigwa, ambazo zinamuonyesha akiwa mbele katika kaunti 14 kati ya 15.
'Tunasubiri tangazo la ushindi'
"Kwa sasa, nadhani kiongozi wetu George Weah yuko katika nafasi ya ushindi, kwa hivyo tumesimama, tunasubiri tume ya uchaguzi kutupa matuokeo," alisema mfausia wa Weah Francis IT, mfanyabiashara mjini Monrovia.
Katika mahojiano nyumbani kwake nje kidogo ya mji mkuu wa Liberia Monrovia, Boakai alisema anadhani atashinda. Lakini alionyesha wasiwasi iwapo uchaguzi huo utakuwa huru na wa wazi.
Weah, mwanasoka pekee wa Kiafrika aliewahi kuchaguliwa kuwa mwanasoka bora wa shirikisho la Kandanda duniani FIFA, alikuwa akipewa nfasi kubwa ya kuibuka mshindi na kumrithi rais anaemaliza muda wake, mshindi wa tuzo ya Nobel Ellen Johnson Sirleaf.
Liberia ndiyo jamhuri kongwe zaidi barani Afrika, na ilianzishwa na watumwa walioachwa huru kutoka Marekani mnamo mwaka 1847. Makabidhiano yake ya mwisho ya madaraka kwa njia ya kidemokrasia yalitokea mwaka 1944, na yalifuatiwa na mapinduzi ya kijeshi mwaka 1980 na vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyodumu kwa miaka 14, na kumalizika tu mwaka 2003.
Mwandishi: Iddi Ssessanga/rtre,afpe
Mhariri: Daniel Gakuba

www.ngarakwetu.blogspot.com

December 16, 2017

UCHAGUZI WA ANC,AFRIKA YA KUSINI

Ramaphosa, Dlamini-Zuma kuwania uongozi wa ANC

SOURCE:DW
Chama tawala nchini Afrika kusini,  ANC kinafanya uchaguzi mwishoni mwa juma, unaoonekana kuwa mgumu, kumchagua mrithi wa kiongozi wake Jacob Zuma, ambapo mshindi  pia atakuwa na nafasi ya kuwa  rais mpya wa nchi hiyo.
Bildkombo Nkosazana Dlamini-Zuma und Cyril Ramaphosa (Getty Images/AFP/R. Jantilal/G. Kirk)
Chama  cha  ANC  kitamtangaza  mrithi  wa  rais  wa  sasa  Zuma kuwa  kiongozi  wa  chama  Jumapili (17.12.2017), kikikamilisha mpambano  mkali  wa  kuwania  uongozi  ambao unatishia  kukigawa chama  hicho  ambacho  kilianza  kama  vuguvugu  la  ukombozi miaka  105  iliyopita, ambacho  kimekuwa  madarakani  tangu mwaka  1994.
Makamu  wa  rais Cyril Ramaphosa , mwenye  umri  wa  miaka 65, ambaye  kwa  kiasi kikubwa  anapendelewa  na  masoko  ya  fedha, na  Nkosazana Dlamini-Zuma, mwenye  umri  wa  miaka  68, waziri  wa  zamani  na mwenyekiti  wa  halmashauri  ya  Umoja  wa  Afrika  wametamalaki katika  mpambano  huo.
Cyril Ramaphosa Südafrika Wahlen (DW/A. Lattus)
Makamu wa rais Cyril Ramaphosa
Sarafu  ya  Afrika  kusini  ya  rand imekuwa  imara  kwa  asilimia mbili  baada  ya  mahakama  kutoa  hukumu  kwamba maafisa waandamizi  katika  majimbo  mawili walioonekana  kumuunga mkono  Dlamini-Zuma walichaguliwa  kinyume  na  sheria  na hawataruhusiwa  kuhudhuria  mkutano  huo.
"Ishara  za  mapema za ushindi  kwa  Cyril Ramaphosa, ambaye anapendelewa  na  wawekezaji  zaidi, ametoa  usaidizi kwa  sarafu ya  rand," John Ashbourne , mtaalamu  wa  uchumi  wa  Afrika  katika taasisi  ya  Capital Economics  amesema.
"Lakini  wakati Ramaphosa anaungwa mkono  kwa  kiasi  kikubwa miongoni  mwa  wanachama  wa  chama  hicho, matokeo yataamuliwa  na  watu  wa  ndani kisiasa, ambao  huenda wakaamua  kumuunga mkono  mpinzani  wake mfuasi  wa  siasa  wa mrengo  wa  kushoto, Nkosazana Dlamini-Zuma.
Dlamini-Zuma (Getty Images/AFP/F. Monteforte)
Nkosazana Dlamini-Zuma
Ramaphosa  alishinda  kwa  wingi  wa  kura  za  kuteuliwa  kuwa kiongozi  wa  chama, lakini  wajumbe  katika  mkutano  huo ulioanza JumamosiDisemba  (16-12  hadi 20.12.2017) mjini  Johannesburg hawafungwi na kura alizopigiwa  na  tawi la  chama  cha  ANC lililomteua  kuwa  mgombea  wao, ikiwa  na  maana  kwamba  bado haiko  wazi  iwapo  anaweza  kushinda  nafasi  hiyo.
Ramaphosa  ameongeza  hivi  karibuni  ukosoaji  wa  serikali  ya Zuma  iliyogubikwa  na  kashfa, wakati Dlamini-Zuma  amesema umuhimu   wake  anauweka  katika  kuboresha  uwezo  wa  Waafrika waliowengi.
Waungaji mkono Ramaphosa
Kwa  waungaji  wake  mkono, mafanikio  ya  Ramaphosa  kibiashara yanamfanya  kuwa  katika  nafasi  nzuri  ya  jukumu  la  kubadilisha hali  ya  uchumi  wa  nchi  hiyo  inayokabiliwa  na  ukosefu  wa nafasi  za  ajira  kwa  asilimia  28  ya  watu pamoja  na kupunguziwa viwango  vya  uwezo  wa  kukopa.
Südafrika Zuma hält Rede im Orlando Stadion in Soweto (Getty Images/AFP/M. Safodien)
Mkutano wa ANC akihutubia mwenyekiti Jacob Zuma
Kwa upande  mwingine, Dlamini-Zuma anaonekana  kuwa  mpiganaji imara  dhidi  ya  kutokuwa  na  uwiano  wa  Waafrika  na  wazungu hali  ambayo  uhasama  wake  unaoelekezwa  katika  makampuni makubwa  umewatisha  wawekezaji   nchini  Afrika  kusini.
"Matokeo  ni  vigumu  kutabiri. Hii  inaleta  hali  mbaya  ya sintofahamu  ambayo  inaakisi  kwa  kiwango  kikubwa  hali  mbaya ya  sarafu  ya  rand, " Elizabeth Andreae, mchambuzi  katika  benki ya  Commerzbank  amesema  katika  taarifa.
Ukuaji  wa  uchumi  katika  taifa  hilo  lenye  uchumi  mkubwa  wa viwanda  barani Afrika umekuwa  wa  kusua sua  kwa  miaka  sita iliyopita, na  kiwango  cha  watu  wasio  na  kazi  inakaribia  viwango vya  juu  kabisa.
Wachambuzi  wanasema  kinyang'anyiro  cha  kuwania  uongozi  wa ANC  umefanya  hali  kuwa  ngumu  kuweza  kufanya  mabadiliko  ya kiuchumi  na  kuboresha  huduma  za  jamii.
Ruanda Rede Nkosazana Dlamini-Zuma Sitzung AU Gipfel (picture-alliance/Photoshot/P. Siwei)
Rais wa zamani wa halmashauri ya Umoja wa Afrika Nkosazana Dlamini-Zuma
Zuma alitoa utani  katika  chakula  cha  usiku  kwa  wajumbe  wa ANC katika  mkesha  wa  mkutano  huo  mkuu  na  kusema  kwamba "imekuwa uzoefu unaostahili" na  kwamba  anasubiri  kwa  hamu kuondoka  madarakani  kama  kiongozi. Anatarajiwa  kutoa  hotuba yake  ambayo  si  rasmi  sana  mwanzoni mwa  mkutano  huo  mkuu wa  chama. Anabakia  kuwa  kiongozi  wa  taifa  hadi  2019.
Rais  huyo  mwenye  umri  wa  miaka  75 amekana  madai  kadhaa ya  rushwa  tangu  alipoingia  madarakani  mwaka  2009  na amenusurika  mara  kadhaa  katika  kura  za  kutokuwa  na  imani nae  bungeni.
"Watu wanasubiri  kwa  hamu  kuondoka  kwake," mchambuzi  wa masuala  ya  kisiasa  Prince Mashele  amesema  katika  taarifa yake  aliyoiandika  katika  gazeti  moja.
Mwandishi: Sekione Kitojo / rtre
Mhariri: Isaac Gamba
www.ngarakwetu.blogspot.com

December 7, 2017

TUPAMBANE NA HALI

Tulio wengi tumepitia hali hii. Si haki yetu kuwa hivi, Tuna kila hali ya kupambana na hali hiyo. Nakaribisha mawazo kwenu ndugu jamaa na marafiki, wafuasi wa blogu hii. Tufanye nini kusaidia watoto waliopo katika hali ya nama hii?
Niandikie juveilla@gmail.com au piga simu no. 0743046811
www.ngarakwetu.blogspot.com

August 14, 2017

KARIBU THE MSANII ARTIST

-Tuna Print T-Shirt,Kuuza na Kuchapa kwa Mashine(Aina zote za T-shirt)Nguo za shule na Vifaa vya Michezo..

-Tunachora na Kuandika Mabango aina zote.

-Tunatengeneza mawe ya msingi,Ufunguzi na Uzinduzi aina zote na za kisasa.

-Tunatengeneza nembo na kutoa mafunzo ya sanaa za mikono kwa mtu mmoja mmoja.

Kauli mbiu yetu kuelekea Tanzania ya Viwanda "Fanya Kazi nasi,Epuka Vishoka"

Tunapatikana Geita Mjini Mtaa wa NMB kona ya kuelekea Hospitali ya Mkoa, na Kasulu tupo mtaa wa Mahwenyi karibu na Neema Guest House


Kwa mawasiliano zaidi....0756 54 40 01/ 0784 544 001 na 0754 676 830. Huduma zetu zinaweza kukufikia popote ulipo.
    Wote Mnakaribishwa



                            www.ngarakwetu.blogspot.com

June 30, 2017

Ujenzi wa Vyumba vya Madarasa,Mabweni na Matundu ya vyoo




Mbunge wa jimbo la Ngara Alex R.Gashaza akikagua ujenzi wa Vyumba vya Madarasa,Mabweni na matundu ya Vyoo katika Shule ya Sekondari Murusagamba.
Picha na Issa Kazimoto-Dereva wa Mbunge

www.ngarakwetu.blogspot.com

Mbunge wa Ngara,atoa vifaa vya Michezo

Mbunge wa jimbo la Ngara Alex R.Gashaza ameta Vifaa vya michezo ikiwemo mipira na Jezi kwa wachezaji wa timu 78 zilizoshiriki ligi yake maarufu kama Gashaza Cup mzunguko wa vijiji,kuelekea kata na sasa hatua inayofuata ni tarafa kutafuta mshindi wa wilaya.
Picha na Issa Kazimoto,dereva wa Mbunge





Pichani,Mbunge wa jimbo la Ngara Alex Gashaza katika matukio tofauti ya kukabidhi vifaa vya Michezo.
www.ngarakwetu.blogspot.com

June 25, 2017

UZINDUZI WA DAYOSISI BIHARAMULO,ASKOFU WA KWANZA VITHALIS YUSUPH SUNZU




Askofu Mkuu wa Kanisa la Anglikan Tanzania Dk.Jacob Chimeledya ametaka serikali kufanya marekebisho  baadhi ya sheria ambazo zimekuwa kandamizi kwa jamii pamoja na kuiangazia upya  mikataba yote inayohusu rasimimali za umma yakiwemo madini ili ziwe na manufaa kwa wananchi.

Askofu Chimeledya ametoa kauli hiyo  kwenye ibada ya kuzindua dayosisi Mpya ya Biharamulo na kuwekwa Wakfu kwa Askofu wa kwanza wa Dayosisi hiyo Askofu Vithalis Yusuph.

Bila kutaja sheria husika ,Alisema baadhi ya sheria zikiwemo sheria paamoja na mikataba iliyoingiwa na serikali inaumiza wananchi na hivyo ifaa ifanyiwe marekebisho ili rasilimali hizo ziwanufaishe wananchi.

Alisema Tanzania bado ina mikataba mibovu hasa katika sekta ya madini kwani rasilimali hizo haziwanufaishi wananchi kama zilivyotolewa na mwenyezi Mungu kwa ajili wanadamu.

Alishauri serikali kuwa, kama kuna mikataba iliyoingiwa ni mibovu heri ikafanyiwa marebisho kuliko kuendelea kupoteza rasilimali nyingi za watanzania kwa manufaa ya watu wachache.

Aidha kusuhu sheia za mwanamke Askofu huyo alisema katika sheria nyingine mbovu ni sheria ya motto hasa wa kike ambapo baadi yake zimekuwa kandamizi kwa motto wa kike kwani zimekuwa hazimlindi mtoto wa kike katika mazingira ya leo na hivyo kuwa kandamizi kwake.

“Tunaomba sheria zirekebishwe zikiwemo za kulinda haki za mtoto wa kike katika mazingira ya leo.Tunaona baadhi ya sheria haziendani kabisa na utu wa kibinadamu na zimekandamizi kwa mtoto hasa wa kike”alisema Askofu.

Hata hivyo,alisema kanisa linaunga mkono juhudi za serikali inayoongozwa na Rais John Pombe Magufu katika kupigania rasilimali za nchi yakiwemo madini,na kuongeza kuwa kanisa litaendelea kumuombea.

“Tunatambua kazi nzuri zinazofanywa na rais Wetu Magufuli za kupigania rasimali za nchi,lakini cha msingi tunaomba kasoro zilizopo kwenye mikataba ya madini na sheria zingine mbovu zifanyiwe marekebisho…zipo kanuni nyingi ambazo zimetumifika hapa tulip oleo”alisema Askofu.

Aidha,Askofu wa Dayosisi ya Biharamulo katika Hotuba yake mara baada ya kusimikwa kuwa Askofu wa Dayosisi hiyo ya 28,alisema Watanzania walio wengi wanaishi katika mazingira magumu na ili kuondokana na hali hiyo Viongozi wa dini na serikali wana wajibu wa  kuwahudumia wananchi kwa ushirikiano.

Katika kuonyesha kukerwa na tabia za utumikishwaji wa watoto,Askofu Yusuph alisema, kanisa la Angilikani Dayosisi ya Biharamulo halitakubali kuona motto anatumikishwa katika ajira hatarini za migodini,kwenye migahawa na kuchunga mifugo.

Akizungumzia changamoto za wananchi wa Biharamulo mbele ya Mgeni Rasim Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga,alisema wakazi wa wilaya hiyo wanakabiliwa na tatizo la upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama.

Alisema kutokana na hali hiyo baadhi yao wamekuwa wakishinda usiku wamanane wakitafuta huduma ya maji sehemu mbalimbali na hata maji wanayotumia hayako salama kwa ajili ya Afya zao.

Aliongeza kuwa kanisa litashirikiana na serikali kuhakikisha huduma ya maji safi na salama kutoka Ziwa Victoria inapatikana kwani kanisa hilo linatambua juhudi za serikali za kuwaletea wananchi maendeleo.

Kwa upande wake Mgeni Rasmi Ezekiel Kyunga ambaye pia ni Mkuu wa mkoa wa Geita aliyemwakilisha Rais wa John Pombe Magufuli katika Hafla hiyo alisema,serikali itahakikisha inashughulikia kero za wananchi na kuwataka viongozi wa dini kutoa ushirikiano katika mkakati wa serikali ya awamu ya tano ya kuwaletea wananchi maendeleo.

Amewataka vongozi dini kuhakikisha wanatumia nafasi zao katika kueneza injili ili kuwa Taifa lenye kumpendeza Mungu na kupunguza uharifu unaojitokeza.

Kuhusu maji,alisema serikali iko tayari kushirikiana na kanisa hilo kuhakikisha wananchi wa Biharamulo wanapa huduma ya maji safi na salama,na kudai kuwa anatambua juhudi za kanisa hilo kutumia rasilimali fedha kuwahudumia wananchi ikiwemo elimu,Afya na Maji.

Shughuli za kusimikwa kwa Askofu huyo zilifanyikwa kwa kuzingatia miongozo ya kanisa hilo ikiwemo kula kusoma hati mbalimbali za viapo ili kulitumikia kanisa hilo.

Hafla hiyo ilihudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa dini kutoka dayosisi za Tanzania viongozi wa serikali wakiwemo wakuu wa wilaya pamoja waumini wa dayosisi za Biharamulo na Kagera.
Mwisho


www.ngarakwetu.blogspot.com